Chem chem Association yakabidhi maboma 15 kwa wafugaji Manyara.
1 August 2024, 2:42 pm
Kutokana na uwelewa mdogo wa wafugaji namna ya kulinda mifugo yao ili isivamiwe na wanyama wakali serikali itaendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau ili kujenga maboma hai mengine na kulinda wanyama wanaofugwa na binadamu .
Na Marino Kawishe
Taasisi ya Chem chem Association imekabidhi maboma hai 15 kwa baadhi ya wafugaji wanaoishi pembezoni mwa jumuiya ya ya hifadhi ya wanyama pori Burunge kutoka vijiji vya ngoley, vilima vitatu na Sangaiwe kwa lengo lakukabiliana na wanyama wakali ikiwemo Simba.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngoley katibu tawala Wilaya ya Babati Halfan Matipula Amesema serikali itaendelea kutoa elimu na kushirikiana na wadau kujenga maboma hai zaidi ili kuendelea kulinda wanyama wanaofugwa na binadamu kwa ujumla.
Kwa upande wake Msimamizi wa miradi ya maendeleo kwa jamii kutoka Chem chem Association Napendaeli Wazoel amesema kila boma zimegharimu kiasi cha zaidi ya shilling milion mbili na lengo nikuhakikisha wananchi wanaoishi pembezoni ya hifadhi mifugo yao inakuwa salama