Wajasiriamali tumieni masoko Kimataifa
25 June 2024, 4:06 pm
kutokana na Soko la ndani kuwa huru wanawake wajasiriamali mkoani Manyara wametakiwa kuzingatia ubora wa bidhaa wanazo zalisha Ili kuendeleza masoko ya ndani na nje ya nchi ili kuwainua kiuchumi kutokana na fursa zilizopo.
Na Angela Munuo
Wanawake wajasiriamali wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kuongeza thamani ya bidhaa zao ili kuyafikia masoko ya kimataifa na kujikwamua kiuchumi kutokana na biashara mbali mbali wanazozifanya.
Akifungua mafunzo ya wanawake wajasiriamalii june 24 katika ukumbi wa Goodlife mkoani hapa mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Jacob Twange amesema mafunzo hayo yatafungua milango kwa wajasiriamalii kufanya biashanya ndani na njee ya nchi kutokana na bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali na kuwataka kuzingatia ubora wa bidhaa wanazozalisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya Chama cha wafanyabiashara Tanzania (TWCC) ambaye ni mratibu kanda ya kaskazini Joyce Ndosi amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia elimu wanawake wajasiriamalii na kuwakuza kiuchumi kwa kuwapa elimu ya kuongeza thamani katika bidhaa zao ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo kufanya biashara zao katika soko huru la Africa .
Aidha,wajasariamali wadogo walihudhuria mafunzo hayo, wamesema wamefurahishwa na mafunzo hayo pamoja na elimu iliyotolewa ya kuyafikia masoko ya kimataifa na wamewataka wanawake wenzao wajasiriamalii kuchangamkia fursa zilizopo ili kufanya biashara kwakua masoko yapo na yataweza kuwainua kiuchumi.