FM Manyara

Manyara yatajwa kuwa na asilimia 32 ya udumavu

25 June 2024, 1:29 pm

Picha ya Afisa elimu lishe kutoka TAHA Jaqline Maramoko akitoa elimu ya umuhimu wa lishe bora

Licha ya mkoa wa Mnyara kuwa na uzalishaji mkubwa wa vyakula mbali mbali hali ya udumavu imeonekana kuwa juu hasa katika maeneo ya kata ya Bashay iliyopo wilaya mbulu vijijini

Na Marino Kawishe

Mkoa wa Manyara umetajwa kuwa na silimia 32 ya udumavu ambapo wananchi  wametakiwa makundi yote sita ya vyakula ili kundokana na hali hiyo ya udumavu ambayo imekithiri kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Mbulu Veronica Kessy alipokuwa akitoa hotuba ya mgeni rasmi kwenye kilele cha siku ya Lishe Mkoa wa Manyara kilichofanyika  kijiji cha Langangesh ambacho kinachoongoza kwakuwa wananchi wenye udumavu katika wilaya hiyo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mbulu

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Salome Francis, amesema jamii ya Watanzania inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa lishe bora na imepelekea magonjwa mengi kuendelea kushamiri kwenye jamii zao.

Kwa upande wake kaimu  Mkurugenzi mkuu wa TAHA  Nchini Antony Chamanga amesema TAHA wataendelea kushirikiana na wakulima mbali mbali ili kuboresha mazao ya chakula na kwa wilaya ya Mbulu wanatarijia kuanza kutoa elimu ya kilimo cha parachichi na kitunguu swaumu ambayo yanalimwa kwa wingi katika eneo hilo na nimazao ambayo yanaongeza kipato kwa wananchi.

Sauti ya kaimu Mkurugenzi Mkwa Taha

Aidha Afisa elimu lishe kutoka TAHA Jaqline Maramoko ameitaka jamii kutumia mazao yenye lishe kama mazao yenye ukijani kubaki na rangi yake ili kuendelea kupata virutubisho ambavyo vinapatikana katika makundi sita ya vyakula.

Sauti ya Afisa elimu lishe kutoka Taha

Maadhimisho  ya siku ya Lishe kimkoa yamefanyika  wilayani Mbulu mkoani Manyara na kauli mbiu ya mwaka 2024 “LISHE BORA KWA AFYA NJEMA NA USTAWI WA TAIFA”.