Watoto milioni 5.1 wanatumikishwa nchini
4 June 2024, 6:23 pm
Mikoa ya Mwanza, Simiyu na Shinyanga yaongoza kwa utumikishwaji wa watoto nchini kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na mikoa mingine ambapo elimu inahitajika kutolewa kwa jamii.
Na Marino Kawishe
Kuelekea siku ya kupinga utumikishwaji kwa watoto serikali imetakiwa kukomesha utumikishwaji wa watoto katika maeneo mbalimbali nchini ambapo takwimu zinaonyesha watoto milioni 5.1 kuanzia miaka 5 hadi 17 wanajishughulisha na kazi zisizokuwa rasmi kwa watoto.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kupinga utumikishwaji kwa watoto Ibrahimu Isamaka alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema mikoa inayoongoza kuwa kwa utumikishwaji wa watoto kwa kiwango kikubwa hapa nchini ni Mwanza, Simiyu na Shinyanga.
Aidha, mjumbe wa kamati kutoka mtandao wa mashirika dhidi ya utumikishwaji watoto Tanzania (TCACI) Irene Sitoti amesema katika kuadhimisha siku hiyo wataadhimisha kwa kutoa elimu na kuweka mijadala mbalimbali pamoja na kushirikisha mashirika ya kimataifa na kila mwaka kutakuwa na mjadala wa kitaifa kwa kushirikiana na serikali ili kutokomeza utumikishwaji kwa watoto nchini.