Polisi Manyara watumia mabomu ya machozi kutawanya wananchi
21 February 2024, 5:57 pm
Jeshi la polisi mkoani Manyara lalazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi walioandamana bara bara kuu ya Babati -Arusha kufuatia kuuliwa kwa mtoto wa miaka saba
Jeshi la polisi mkoani Manyara limelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi waliokuwa wameandamana katika bara bara kuu ya Babati –Arusha wakizuia magari ya abiria kupita kufuatia kuuliwa kwa mtoto wa miaka saba
Wananchi hao wa kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara, wamesema wamelazimika kuandamana hadi katika kituo cha polisi cha Magugu wakipinga jeshi la polisi mkoani hapa kumpeleka mtuhumiwa kituo cha polisi nakutaka kumuua kwakua watuhumiwa wengi wanaachiwa huru.
Aidha kufuatia ghasia hizo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara George Katabazi amelazimika kuongeza nguvu ya maaskari ili kutuliza wananchi na kupata suluhu ya kuzungumza nao kwa njia ya amani huku akielezea kilichojiri katika eneo la tukio.
Mapema asubuhi kamanda Katabazi alifika katika kijiji hicho kutoa pole kwa wanafamilia, na kuahidi jeshi la polisi halitamfumbia macho mtuhumiwa yeyote atakaehusika na vitendo vya kiharifu katika kata hiyo ya Magugu na kutoa gari katika kituo cha polisi Magugu ili lisaidia kuimarisha hali ya ulinzi na usalama.