Mageuzi yafanyika sekta ya kilimo Manyara
7 November 2024, 6:36 pm
Serikali imetoa zaidi ya shilling trillioni moja ili kuboresha sekta ya kilimo nakumpunguzia mkulima gharama katika kilimo kwa kupata ruzuku ya mbegu za mahindi
Na Angel Munuo
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka waingizaji,wauzaji wasambazaji na mawakala wa mbegu za mahindi kuuza mbegu kwa bei elekezi ya ruzuku ambayo imeelekezwa na serikali na ipo katika miongozo.
Sendiga ameyasema hayo ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari amesema mageuzi yamefanyika katika sekta ya kilimo kwa kuweka ruzuku katika begu za mahindi ili kuwasaidia wakulima kuwa na uhakika wa chakula na mazao.
Aidha Sendiga amesema serikali imetoa zaidi ya shilling trillioni moja ili kuboresha sekta ya kilimo nakumpunguzia mkulima gharama katika kilimo kwa kupata ruzuku ya mbegu za mahindi ambapo bei ya mbegu ya mahili kwa kilo mbili itauzwa kwa shilingi elfu kumi na mbili ambapo awali ilikuwa inauzwa kwa shilingi elfi kumi na tisa.
kwa upande wake katibu tawala msaidiziFaraja Ngerageza anayesimamia sehemu ya uchumi na uzalishaji amesema serikali ya awamu ya sita imeweka ruruku katika mbegu zamahindi kwa wakulima ili kumpunguzia gharama mkulima aweze kulima kwa tija na kujihakikishia usalam wa chakula.