FM Manyara

Mshauri (TCCIA ) Manyara kizimbani

24 March 2024, 1:34 pm

Picha ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara.

Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara ya muachia huru Mshauri wa Wafanyabiashara TCCIA

Na Mzidzlifa zaid

Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara imemhukumu  Ramadhani Rashid Msangi Mshauri wa Wafanyabiashara wa Chama cha wenye viwanda na kilimo Mkoa wa Manyara (Bussines consultant -TCCIA Manyara) kwenda jela miaka mitatu au kulipa kiasi cha shilingi 900,000 kwa kosa la kughushi  nyaraka  za malipo .

Hukumu hiyo dhidi ya Ramadhani Rashid Msangi katika shauri la uhujumu uchumi na. 05/2023, imetolewa na hakimu Mkazi wa Mahakama  ya Manyara Martin Massao Machi 22, 2024.

Hakimu Massao amesema Mshtakiwa huyo  alighushi nyaraka mbali mbali katika marejesho yake  kuonyesha kuwa alihudhuria  na kuendesha mafunzo ya wajasiriamali yaliyofanyika wilayani Hana’ng mkoani Manyara kwa kipindi cha mwezi februari  na juni mwaka 2018 ambapo alitumia kiasi cha shilingi 6,695,000  Kugharamia posho ya chakula , ukumbi na nauli kwa waliodaiwa kushiriki mafunzo hayo na akijua taarifa hizo hazikuwa sahihi.

Aidha,mshitakiwa  amelipa  faini na kuachiwa huru na mahakama hiyo.