Radio Jamii Kilosa

Wazazi hakikisheni watoto wanapata elimu

31 January 2023, 12:16 pm

Katibu Mkuu CCM Comrade Daniel G. Chongolo katika ziara yake ya kufatilia utekelezaji wa ilani ya CCM wilayani Kilosa.Picha na Gladys Mapeka

Wazazi na walezi watakiwa kuhakikisha watoto wao wanapata elimu ambayo inatolewa bila malipo pamoja na kuwalea katika maadili mema kwa kuwarithisha mila na desturi njema ili kuwa taifa lenye sifa njema na maadili mema.

By Asha Mado

Katika kuhakikisha watoto wanapatiwa haki ya elimu Katibu Mkuu CCM Comrade Daniel G. Chongolo katika ziara yake ya kufatilia utekelezaji wa ilani ya CCM ambapo amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata elimu ambayo inatolewa bila malipo.

“Mtoto anapopata elimu inamsaidia kupata fursa mbalimbali katika ajiraComrade Chongolo amesema kuwa watoto wanapopata elimu ni rahisi kuingia katika sekta mbalimbali ili kujipatia ajira kwani ili kizazi cha sasa kiweze kuwa cha ushindani alisema Comrade Daniel Chongolo.

Aidha katika ziara yake ametembelea katika shule za sekondari za Maguha na Mikumi  na kuwapatia zawadi ya jezi na mipira miwili toka kwa Mheshimiwa Rais wa awamu ya sita kwa shule zote mbili ambapo pia ametaka kukamilishwa kwa miundombinu ya nishati ya umeme ambayo haijakamilika ili nishati ya umeme iweze kupatikana katika shule ya sekondari ya Maguha ambayo ni mpya, ambapo pia amewapongeza wananchi wa Kilosa kwa juhudi wanazofanya katika kujiletea maendeleo kwa kushiriki shughuli za maendeleo.

Pamoja na hayo ametaka wanakilosa kuunga mkono juhudi mbalimbali zilizofanywa na Serikali kwa kutunza miundombinu mbalimbali iliyopo ndani ya wilaya kwa kuhakikisha inatunzwa ili iweze kutumika kwa muda mrefu huku upande wa mashamba yaliyofutwa na Mheshimiwa Rais amesema Waziri wa kilimo atafika wilayani Kilosa ili kusikiliza wakulima ili yaweze  kutolewa maamuzi sahihi dhidi ya changamoto za wakulima katika matumizi sahihi ya mashamba hayo.