Radio Jamii Kilosa

Ujenzi wa Vituo vya afya na sekondari Kilosa ukamilike desemba mwakahuu-Prf Shemdoe.

8 September 2021, 2:58 am

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe ameagiza kuharakishwa kwa ujenzi wa vituo viwili vya afya vilivyopatiwa fedha mwaka huu 2021/2022 kiasi cha shilingi milioni mia tano kila kituo pamoja na shule ya wasichana Sekondari iliyopatiwa bilioni moja ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

Agizo hilo limetolewa Septemba 6 mwaka huu wakati Katibu Mkuu akizungunza na watumishi wa kada mbalimbali katika Chuo cha Ualimu Ilonga wilayani Kilosa.

Prof. Shemdoe amesema Serikali inapoleta fedha kwa ajili ya miradi ni lazima miradi hiyo itekekezwe kwa wakati ili kuwaletea wananchi maendeleo ambapo kutokana na kuchelewa kuanza kwa miradi hiyo amemuagiza Katibu Tawala Mkoa kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi hiyo.

Aidha katika mwaka huu amesema Serikali itaiongezea Wilaya ya Kilosa vituo viwili vya afya kwa kuwa ina majimbo mawili ya uchaguzi ambapo ameagiza shilingi bilioni moja zianze kutumika moja ili huduma stahiki ziweze kutolewa kwa wananchi.

Akizungumzia kero za watumishi zilizowasilishwa kwake ikiwemo uhaba wa watumishi amesema tayari mhandisi na mkaguzi wa ndani wameshapelekwa nakwasasa aiangalia ofisi ya manunuzi wanaoonekana kukwamisha mchakato wa manunuzi.

Katika hatua nyingine amewataka watendaji wa kata na maafisa tarafa kusaidia kazi za ujenzi wa mirado ya maendeleo ili kufikia malengo ya kutoa huduma kwa wananchi na kuzingatia matumizi ya force ya force account huku akikemea vikali vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya maafisa kwani jambo hilo halivuliki ma atakayebainika atachukuiiwa hatua.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa Morogoro Bi. Mariam Ntunguja amemshkuru Katibu Mkuu kwa kupokea kero na ushauri toka kwa watumishi huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kisena Mabuba amesema Halmashauri amesema Halmashauri imejiwekea malengo ya kukusanya zaidi ya aslimia 80 ya mapato ya ndani ya lengo la makusanyo kwa mwaka jambo litakalowezesha shughuli za maendeleo