Radio Fadhila
Radio Fadhila
27/03/2026, 13:48

Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) @etdco_tz imeendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia maalumu ya kusafirisha umeme yenye urefu wa kilomita 76 kutoka wilaya ya Masasi hadi Newala, mkoani Mtwara.
Mradi huu ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuboresha upatikanaji wa nishati ya uhakika katika ukanda wa kusini. Lengo kuu ni kuimarisha miundombinu ya usafirishaji wa umeme, kupunguza upotevu wa nishati, na kuongeza uwezo wa kusambaza umeme kwa wananchi na shughuli za kiuchumi katika Wilaya za Masasi, Newala, na vitongoji jirani.
Akizungumza kuhusu maendeleo ya mradi huo, mmoja wa wahandisi wanaosimamia utekelezaji wake amesema kuwa kazi inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa.
Aidha, alisema kwamba kukamilika kwa mradi huo kutachochea ukuaji wa viwanda vidogo na vya kati, pamoja na kuboresha huduma za kijamii kama afya na elimu.