Radio Fadhila

Madiwani Masasi wakoshwa na msimamizi wa miradi

11 February 2026, 1:28 PM

Katika ziara ya ukaguzi wa miradi

Madiwani wa Halmashauri ya Mji Masasi wamempongeza Mkurugenzi wa Mji Ndg Reuben Jichabu na menejimenti kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.1 ambayo inatekelezwa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani na fedha kutoka Serikali Kuu.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara maalumu ya Waheshimiwa Madiwani wote ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi Mhe.Sospeter Nachunga amesema ameridhishwa na kasi ya miradi pamoja na thamani ya fedha ambayo imetumika katika utekelezaji wa miradi hiyo huku akiipongeza menejimenti na Mkurugenzi wa Mji Masasi kwa kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo fedha zake zimeingia kipindi ambacho Baraza la Madiwani lilikuwa limevunjwa.

Ziara hiyo imetembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya wodi ya VVIP Mkomaindo ,Soko Mbadala Mkuti,Machinjio ya kisasa,Mradi wa Ghala ,ujenzi wa Madarasa manne na matundu ya vyoo shule ya msingi kambarage ,ujenzi wa shule ya mkondo mmoja Anna Abadallah pamoja na madarasa ya mawili ya awali na matundu ya vyoo shule ya msingi