Radio Fadhila
Radio Fadhila
11 February 2026, 1:13 PM

Kutembea umbali mrefu kufuata shule ilipo hii ni changamoto ambayo wakati mwingine huzima ndoto za watoto kutokana na adha wanazo kutananazo wakiwa njiani lakini inapotokea kuwepo na shule mahali panapofikika kwa urahisi hii uleta furaha si kwa watoto tu hadi wazazi, hivyo ndiyo ilivyokuwa kwa wazazi na viongozi wa kata ya Napupa.

Ujenzi wa shule mpya ya awali na msingi ya mkondo mmoja katika eneo la shule ya sekondari Anna Abdallah kata ya Napupa Halmashauri ya Mji Masasi unatarajiwa kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi pamoja na wingi wa wanafunzi katika shule za jirani ndani ya kata hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa Miradi ya maendeleo ulifanywa na Madiwani wa Halmashauri ya Mji Masasi Februari 9, 2026, Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni Diwani wa kata hiyo, Mhe. Sospeter Nachunga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi huo zaidi ya shilingi milioni 314 ili kuboresha mazingira ya ujifunzaji
