Radio Fadhila
Radio Fadhila
8 January 2026, 1:25 PM

Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Masasi cha kupitia taarifa za maendeleo ya taasisi zote za umma, Halmashauri ya Mji na Wilaya kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2025, kimefanyika Januari 6, 2026, na kuonozwa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Rachael Kasanda.
Katika kikao hicho, Chama cha Ushirika MAMCU Ltd kwa upande wa Wilaya ya Masasi kiliwasilisha taarifa ya mwenendo wa chama, hususani katika uzalishaji na biashara ya mazao ya choroko, mbaazi, ufuta pamoja na korosho.Ambapo Meneja wa MAMCU Masasi, Constantine Frances Laula, alieleza mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto mbalimbali zilizojitokeza ndani ya mwaka 2025.
Aidha, Mwenyekiti wa MAMCU LTD , Alhaj Mfaume (Julajula), alitoa shukrani kwa Umoja wa Wanamasasi kwa mshikamano wao mkubwa katika msimu uliopita, akisema umoja huo umechangia mafanikio ya chama na kuimarika kwa ustawi wa wakulima.
@gmmamcultd @halmashauri_mji_masasi