Radio Fadhila

Bibi mwenye miaka 89 aendelea na fani yake hadi sasa

20 May 2025, 8:46 PM

Bibi Stefania akiwa anatengeneza mkeka

Na Lilian Martin

Licha ya umri alionao, Bibi Stefania Mmole amekuwa akifanya shughuli mbalimbali hali inayomfanya kuwa na nguvu tofauti na watu wa umri wake wanaokaa bila kufanya mazoezi.

Stefania Saidi Mmole mwenye umri wa miaka 89 mkazi wa Masasi mkoani Mtwara amekuwa akijishughulisha na kazi za mikono kama kufuma mikeka ambayo wakati mwingine inamuingizia kipato.

Licha ya umri wake kuwa mkubwa amesema siri kubwa inayomfanya kumudu kufanya vitu mbalimbali kama kufuma mikeka na kuangalia mifungo hii ni kwa sababu hapendi kukaa na kutegemea watu wamhudumie kwa sababu ya umri wake hivyo hupenda kufanya shughuli zake mwenyewe kama mazoezi kwake.