Radio Fadhila
Radio Fadhila
19 April 2025, 11:44 AM

Katibu wa NEC, itikadi, uenezi na mafunzo CCM taifa, CPA Amos Makala akihutubia wanachama na wananchi wilayani Masasi. Picha na Godbless Lucius
Si kila gari lililobeba makaa ya mawe ni kwaajili ya kusafirisha kwenda kuuza nje ya nchi, kuna viwanda vingi nchini vinatumia makaa ya mawe ikiwemo kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara.
Na Neema Nandonde
Katibu wa NEC, itikadi, uenezi na mafunzo CCM taifa CPA Amos Makala amesema kuwa si makaa yote ya mawe yanasafirishwa kwenda kuuzwa nje, bali mengine yanasafirishwa kwenda kwenye viwanda mbalimbali vilivyopo nchini ikiwemo kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara April 17, 2025 na wananchi wa wilaya ya Masasi katika viwanja vya Sabasaba ikiwa ni hitimisho la ziara ya siku 10 kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara, MAKALA amesema kuwa hata kuuza makaa ya mawe nje ya nchi ambako kuna uhitaji mkubwa si haramu, kwani inasaidia kupata fedha ambazo zinaendeshea miradi mbalimbali ya maendeleo.
Sauti ya CPA Amos Makala kuhusu makaa ya mawe
Aidha emeeleza kuwa, kuruhusu wawekezaji kwenye miradi mikubwa ya serikali ikiwemo bandari, ni njia moja wapo ya kuboresha utendaji kazi wa miradi hiyo, akitolea mfano bandari ya Dar-es-salaam ambayo utendaji kazi wake kwa sasa umeboreshwa kwa kiasi kikubwa toka ikabidhiwa kwa DP World.
Sauti ya CPA Amos Makala kuhusu bandari
Ikumbukwe kuwa kwenye ziara ya hivi karibuni ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mikoa ya ya kusini, miongoni mwa yaliyozungumzwa ni kile walichoeleza kuwa licha ya mkoa wa Ruvuma kuzalisha makaa ya mawe, hawanufaiki ipasavyo na malighafi hiyo ambayo husafirishwa kwa wingi kwenda kuuzwa nje ya nchi.