Radio Fadhila
Radio Fadhila
11 April 2025, 2:26 PM

Mkuu wa wilaya ya Masasi Bi. Rachel Kassanda akifuatilia baadhi ya matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa mkutano wa hadhara. Picha na Godbless Lucius
Wanafunzi waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2025, asilimia 98 wamesharipoti shuleni na kuanza masomo.
Na Neema Nandonde
Mkuu wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Bi. RACHEL KASSANDA, amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuzidisha jitihada katika kuinua kiwango cha elimu.
Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara, uliofanyika April 7, 2025 katika Uwanja wa Sabasaba uloitishwa na mkuu huyo wa wilaya kwa lengo la kujitambulisha kwa wananchi na kusikiliza kero zao.
KASSANDA amewapongeza wakazi wa wilaya hiyo kwa mwamko walionao kwenye elimu, kwani kwa wanafunzi waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2025, asilimia 98 ya wanafunzi wamesharipoti na kuanza masomo.
Sambamba na hayo amewataka wazazi na viongozi wa dini, kusimamaia malezi yenye maadili kwa watoto ili kuwaepusha na tabia hatarishi ikiwemo mapenzi ya Jinsia moja.
Katika mkutano huo wa hadhara, Mkuu wa wilaya KASSANDA amekabidhi mfano wa hundi ya shillingi million 148 ambazo ni kati ya shilling million 545.5 ambazo zimetolewa kwa vikundi 105 kupitia mikopo ya 10% iliyotolewa na halmashauri ya mji Masasi kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Mkuu wa wilaya ya Masasi Bi Rachel Kassanda, akikabidhi mfano wa hundi ya Shillingi Million 148 kwa wawakilishi wa vikundi vya ujasiriamali. Picha na Godbless Lucius.