Radio Fadhila

Mkulima auwawa na tembo Liwale

25 March 2025, 3:39 PM

Picha na Google

Tukio hilo limeibua hofu miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, huku wakihofia usalama wao kutokana na tembo kuvamia makazi na mashamba yao.

Na Neema Nandonde

Mkulima Abasi Bakari Libunda (62) kutoka Kitongoji cha Nangorokoro, Kijiji cha Mirui Wilayani ya Liwale Mkoani Lindi amefariki baada ya kushambuliwa na tembo akiwa katika shamba lake la ufuta.

Tukio hilo limetokea Machi 24, 2025 majira ya saa 6:00 asubuhi, wakati tembo walipoingia shambani na kumjeruhi vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake.

Daktari Akbar Magonyozi Thomas kutoka Kituo cha Afya Kibutuka, amefanya uchunguzi wa mwili wa marehemu na kuthibitisha kuwa amefariki kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata, baada ya kushambuliwa na mnyama huyo.

Baada ya uchunguzi wa kitabibu, mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa familia kwa ajili ya mazishi.

Tukio hilo limeibua hofu miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, huku wakihofia usalama wao kutokana na tembo kuvamia makazi na mashamba yao.

Aidha wakazi wa kijiji cha Mirui wameiomba serikali na mamlaka husika, kuchukua hatua madhubuti kudhibiti wanyama hao, ili kuzuia madhara zaidi kwa jamii na mali zao.