Radio Fadhila

Jamii yaaswa kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa na meno

18 March 2025, 6:44 AM

Picha na google

“Jamii iachane na msemo wa dawa ya maumivu ya jino ni kuling’oa, kwani siku hizi jino linatibiwa kwanza mpaka ifikie hatua ambayo haliwezekani kabisa ndipo litang’olewa”

Na Neema Nandonde

Kuelekea kilele cha madhimisho ya wiki ya afya ya kinywa na meno, ambacho kitaifa kitafanyika mkoani Mtwara siku ya Machi 20, 2025, jamii wilayani Masasi mkoani humo imeaswa kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa na meno mara kwa mara, ili kugundua tatizo mapema jambo litakalosaidia kupata matibabu kwa wakati.

Redio Fadhila, imefanya mahojiano na mratibu wa huduma za afya ya kinywa na meno wa halmashauri ya mji Masasi, ambaye pia ni daktari wa kinywa na meno kutoka hospitali ya Mkomaindo Dkt Albano Nditi.

Sauti ya sehemu ya kwanza ya mahojiano kati ya Mtangazaji Neema Nandonde na Dkt Albano Nditi kuhusu maadhimisho ya wiki ya afya ya kinywa na meno

Sauti ya sehemu ya pili ya mahojiano kati ya Mtangazaji Neema Nandonde na Dkt Albano Nditi kuhusu maadhimisho ya wiki ya afya ya kinywa na meno