Wanaotarajia kupata mikopo ya 10% wapigwa msasa Masasi
7 January 2025, 10:05 AM
Na Lilian Martin.
Masasi
Vikundi 28 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vinavyotarajia kupata mkopo wa asilimia 10 kutoka Halmashauri ya Wilaya Masasi vimepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya matumizi sahihi ya fedha watakazopatiwa hivi karibuni ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa na serikali.
Pamoja na kufundishwa matumizi sahihi ya fedha, lakini pia wamefundishwa juu ya utawala na uongozi bora, elimu juu ya kuzuia na kupambana na rushwa , usimamizi wa miradi, uendeshaji, ufuatiliaji na usimamizi wa miradi pamoja na ujazaji wa mikataba.
Bw. Shida Chihongaki ni Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Masasi naye ni miongoni mwa walioshiriki katika kuviwezesha kielimu Vikundi hivyo kwenye mafunzo hayo ambapo amesema kwamba jukumu lao la msingi ni kuzuia, kupambana na rushwa “tunazuia kwa Kutoa elimu, tunapambana kwa kumkamata yule ambaye amekiuka miongozo na ndio maana wenzetu wa Halmashauri hapa wametuita sisi katika mafunzo yenu haya tumekuja kuzungumza mapema kabla ya tukio halijatokea, maana tumeambiwa mlianza kwa kuomba, mkaandika maandiko ambayo yamepita katika sehemu mbalimbali ikwemo hata kwetu TAKUKURU yalikuja pia tukayafanyia kazi, na hatmaye vikundi 28 vimepita katika Mchakato na hatmaye leo hii mpo hapa, “..alisema Chihongaki….
aliongeza kwa kusema kuwa
” Wakati tunafanya mchakato wa kupata hivi Vikundi sisi tulikuwa tunapita kuvikagua hivi Vikundi kimoja baada ya kingine ambavyo vinasemekana vinataka mikopo na pia vikundi vya miaka ya nyuma lakini yapo baadhi ya maeneo tumepita na kubaini vikundi hivyo havipo Kabisa (hewa ) yaani watu wamekaa wameandika andiko huku wakisubiria fedha ikitoka wagawane sasa nawashauri fedha ambazo mnaenda kuzipata nendeni mkazifanyie kazi Kama maandiko yenu mlivyoandika ili zoezi lilete tija, na ninahaidi baada hizi fedha Kutoka sisi tutapita kukagua kila kikundi kuhakikisha vinafanya kazi na malengo ya Serikali yanatimia ya kuwainua akina mama, Vijana na watu wenye ulemavu, kwaiyo msiende kufanya tofauti naomba viongozi hakikisheni mnalisimamia hilo na mshirikiane “
Aidha Kamanda Chihongaki akahitimisha kwa kuwaomba wanavikundi hao kuendelea Kutoa ushirikiano kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo inatekelezwa katika maeneo yao kama ilivyokusudiwa kulingana na thamani ya fedha ambayo imetolewa ” Sasa kwenye miradi hapa tusaidiane, miradi ipo kwenu kwenye maeneo yenu, ni yenu hiyo mkiona inakwenda kinyume na utaratibu mtuambie” alisisitiza