Ukaguzi wa miradi mbalimbali wafikia jengo la X-ray Chiwale
3 November 2024, 8:22 PM
Pichani ni jengo la X-Ray
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya Masasi katika ziara yake iliyofanya hivi karibuni ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Halmashauri hiyo imeipongeza Kamati ya Usimamizi wa kituo na Watumishi kwa kazi nzuri inayofanywa katika ujenzi wa jengo la X-ray ambapo wamewataka kuongeza jitihada ili ukamilike kwa haraka na Wananchi waanze kunufaika na huduma hiyo.
Kamati hiyo ikiwa katika Jimbo la Ndanda ikiongozwa na mhe.Amina Mpandula ambaye ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri, Wajumbe ni Mhe.Edward Mahelela, Juma Pole, Kasembe Mponela huku wakiambatana na Wataalamu ambao ni Wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali.
Amesema fedha hiyo ilianza kutumika kwa kufuata muongozo wa matumizi ulipotolewa kwa hatua ya awali mnamo tarehe 19/04/2024 kwa kununua saruji, mawe, mchanga, kokoto pamoja na kununua vifaa vya ujenzi ambavyo kwa ujumla wake iligharimu kiasi cha shilingi Milioni 16,398,000/=
“Hatua ya pili ni ufuatuaji tofali, gharama za Kujenga Msingi na kumwaga zege, gharama za kuchimba Karo na mashimo, gharama ya ujenzi wa boma pamoja na ununuzi wa saruji ambapo hapa jumla ya Shilingi milioni 23,602,00/= zilitumika”..
Hata hivyo pamoja na hayo Bw.Said ameelezea kazi ambazo zinaendelea kwasasa ni Pamoja na kupachika Grill za madirisha, kupachika fremu za milango na kutengeneza blandaring kwa ajili ya siling bodi ambapo jumla ya kiasi cha shilingi Milioni 20,500,000/= kimebaki.
Kituo Cha Afya Chiwale, kipo katika Kata ya Chiwale, tarafa ya lisekese Halmashauri ya Wilaya Masasi, ambapo kituo hiki kinahudumia vijiji 4, Chiwale,Kivukoni,Nanyindwa na ilala huku pia kikihudumia zahanati 9 zinazozunguka kituo.