Radio Fadhila

Mnada wa nne wa Mbaazi MAMCU wauza kwa bei ya sh.1810

1 October 2024, 4:49 PM

Na. Lilian Martin

Chama Kikuu cha ushirika MAMCU kimeuza tani 2536 za Mbaazi katika mnada wa Nne uliofanyika katika Shule ya Sekondari Chiungutwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, bei ya juu ikiwa ni Tsh.1810 na bei ya chini ikiwa ni Tsh.1730.

Mwenyekiti wa MAMCU Ndg. Alhaj Azam Mfaume Julajula akizungumza katika mnada huo amesema ‘Tunashukuru wakulima wamejitokeza kwa wingi na kuridhia kuuza mazao yao na wamefurahia bei ambayo wameipata, Kwetu sisi Mamcu tunashukuru angalau kwa mnada huu na ule uliopita ongezeko la bei limeonekana”.

Ndg.Mfaume ameongeza kwa kusema “ kuanzia mnada wa kwanza mpaka wa tatu Fedha ambazo tumeshaingiza tayari ni zaidi ya Bilioni 25 hivyo niwasihi wakulima wawahi kutoa mizigo na walete magarani kwa haraka ili waweze kuwahi hizi bei”.