Radio Fadhila

Upendo charity yahimiza jukumu la malezi ni jamii

1 July 2024, 8:29 AM

Mkutano wa wanyeviti kata ya nyasa

Katika mkutano wa wenyeviti wa kata ya Nyasa uliofanyika eneo la Maendeleo kwa lengo la kuwaaga wananchi wao katika kata ya Nyasa wilayani Masasi.

Taasisi ya Upendo Charity ilipata nafasi ya kutoa elimu kwa jamii na Bi. Christina Simo alipata nafasi ya kutoa elimu hiyo na kuwakumbusha wazazi na walezi kuhusu jukumu la malezi ni la jamii nzima na kuwataka kuwa macho kwa watoto na kuachana na ukatili kwa watoto kwani mara kadhaa wazazi wamekuwa ‘busy’ na shughuli zao za kila siku na wakiwaacha watoto bila uangalizi wala mahitaji muhimu.

Kwa kusema kuwa hali hii ya wazazi au walezi kuwa bize na mambo yao inayopelekea mtoto kuanza tabia ya uzururaji na kuwa Ombamba hali inayopelekea mtoto kufanyiwa ukatili wa kupigwa,kubakwa,kulawitiwa,kuathirika kisaikolojia.

alisema Bi simo