Radio Fadhila

Wananchi wenye sifa, wazalendo jitokeze kugombea uchaguzi serikali za mitaa

22 June 2024, 5:25 PM

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mtwara DAVID MOLEN amesema katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu ni vizuri Wananchi wenye sifa ikiwemo uzalendo kujitokeza na kugombea nafasi hizo.

Molen ametoa hamasa hiyo wakati akifanyiwa mahojino na mwandishi wa habari mapema wiki hii.

amesema sifa za kugombea nafasi hizo zipo wazi ikiwemo kuwa Raia wa Tanzania, umri unaotakiwa hunashida ya akili unaguswa kutumikia nafasi hiyo, unanguvu unauzalendo na Taifa ni vizuri kugombea.

Molen amezitaja nafasi hizo ni pamoja na wajumbe wa Serikali za Mitaa, Kijiji, lakini pia nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa, Kijiji, na Kitongoji .