Tuaminiane chapongezwa na mwenge wa uhuru
6 June 2024, 7:27 PM
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa 2024 Ndg. Godfrey Eliakimu Mzava amekipongeza kikundi cha vijana cha Tuinuane kilichopo katika kijiji cha Mandiwa ambacho kinajihusisha na ufugaji wa ng’ombe na uuzaji wa maziwa kwa kutoka kukaa tu mitaani na kujiunga kwenye kikundi na hatmaye wakachangamkia fursa ya mkopo kupitia asilimia 10 ya makusanyo ya halmashauri kwenye mapato ya ndani.
Mzava ametoa pongezi hizo mara baada ya mbio za mwenge wa uhuru kutembelea, kuona na kukagua shughuli za ufugaji wa ng’ombe katika kikundi hicho ambapo ametumia fursa hiyo kueleza kuwa lengo la kupatiwa hizo fedha vijana ni kuwawezesha kufanya shughuli zao za kiuchumi na halmashauri ikitakiwa kuwalea, kuwaelekeza na baada ya kuwapatia fedha kuwafuatilia kuona kweli wanafanya hizo shughuli, wanazalisha,wanapata faida, je kuna tija kutokana na shguhuli wanazozifanya.
Mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ya Wilaya ya lpMasasi iliwapatia mkopo wa shilingi 5,000,000/= kupitia fedha za asilimia 4% za mfuko wa Maendeleo ya vijana, na kwa mujibu wa taarifa ya kikundi hicho imeeleza kuwa marejesho ya mkopo huo yamefanyika kwa miaka 2 yaani 2,500, 000/= kila mwaka kuanzia mwaka 2021/2022 na kumalizia mwaka 2022/2023.
Hata hivyo matarajio ya kikundi ni kuongeza ng’ombe wengine na kutoa ajira kwa vijana wengine kupitia mradi huo wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa