Radio Fadhila

Waendesha pikipiki Masasi wapata elimu ya polisi jamii

20 May 2024, 10:02 PM

Inspekta Saada akitoa elimu

Mkaguzi wa Polisi ametoa elimu ya polisi jamii kwa waendesha pikipiki yaani bodaboda katika kata ya Napupa mtaa wa Wapiwapi eneo la standi ya mabasi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Elimu iliyotolewa na mkaguzi huyo Inspekta Saada katika eneo hilo ilikuwa na lengo la kuwakumbusha wajibu wao na kutambua kuwa kazi yao ni ajira kama ajira zingine.

Amewataka bodaboda kuzingatia usalama wao binafsi pamoja na abiria wanaowabeba pamoja na kuhakikiasha wanafuata kanuni na sheria za usalama barabarani kama kuvaa kofia ngumu na kutobeba zaidi ya abiria mmoja na wasitoe vioo kwenye pikipiki zao.

Amewataka pia kushirikiana katika kutoa taarifa za kihalifu kwa wakati sahihi pamoja na kuzingatia alama za barabarani na kuepuka tabia ya kuvipita vyombo vingine vya moto maeneo yasiyostahili kufanya hivyo.