Argentina bingwa wa kombe la Dunia 2022
19 December 2022, 6:56 AM
ARGENTINA BINGWA WA KOMBE LA DUNIA 2022
Pale wazee waliposema ya kale ni dhahabu walimaanisha kabisa hasa ukizingatia kilichotokea kwenye kombe la dunia nchini Qatari historia imeandikwa takribani miaka thelathini na sita nchi ya Argentina kuhusu story ya ushindi wa kombe la dunia chini ya gwiji wa soka Diego Maradona leo dunia imemtambulisha tena gwiji wa soka kwa vijana wa miaka 90 na 2000 tumeshudia akibeba kombe la dunia kiumbe cha ajabu kwenye soka kuwahi kutokea ulimwenguni Lionel Messi .
Kijana mwenzangu pengine hatujamshuhudia Maradona kwa vile ambavyo tunashuhudia ubora wa Lionel Messi akiwa na Argentina leo tunashuhudia umwamba wa Messi kwenye fainali ya kibabe iliyowakutanisha nyota kijana wa Ufaransa Mbape na gwiji wa soka duniani na Argentina Messi .
Naweza sema Messi alistahili hili kombe kwa juhudi yake binafsi na timu kwa ujumla ila kongole kubwa anapewa Messi kwasababu huenda ndio mwisho wa kumuona Mess akicheza kwa ufanisi kwa vile akili na mwili vinafananya kile inahitaji kwa wakati sahihi .
Lionel Scanel alikuwa bora sana kupitia quality ya wachezaji wa Argentina Angle Dimaria ni mkongwe aliyedhihirisha kuwa ya kale ni dhahabu hasa kwa wakati ambao timu inahitaji matokeo ya mechi na si bora mechi game plan ya kocha Lionel ilifanikiwa kupitia yeye Ufaransa wakiwa wengi kwenye defence wanasahau ya kucover nafasi mbele ya Dimaria ambaye anakuadhibu kwa kutengeneza nafasi na kuscore mpango sahihi wa kocha Lionel unaamua mechi mapema kupitia Dimaria setplay na cover space iliwahukumu Ufaransa .
Klyan Mbape quality player anaamua mechi wakati wowote pindi timu ikihitaji huduma yake uwanjani main target kwa Ufaransa na Didier Deschamp ni Mbape na kwenye hili amedhihirisha ubora wake kupitia come back kila movement ya Ufaransa ilikuwa hatari kupitia yeye kiumri ni miaka 23 ila makubwa kwenye world cup anayoyafanya ni rekodi ambayo kijana aliyezaliwa leo atasoma na kushuhudia hili kwa kumtazama zaidi anayo miaka mingi kwenye soka historia ya Lionel Messi na Ronaldo itasalia kwa Mbape na huyu ndiye nyota ajae ukiwatoa Mess na Ronaldo .