Kalinga atimiza ahadi yake kituo cha watoto Excel
11 January 2025, 17:01
MUFINDI
Na Kefa Sika
Mdau wa maendeleo wilayani Mufindi ambaye ni kaimu meneja wa mawasiliano na masoko wakala wa majengo Tanzania TBA Ndugu Fredrick Victory Kalinga amekabidhi magodoro 10 kwenye kituo cha malezi na elimu ya watoto cha Excell kilichopo Mdabulo wilayani humo.
Akizungumza na Mufindi FM 107.3 Ndugu Kalinga amesema kuwa lengo la kutimiza ahadi yake ni kuongeza wigo wa elimu na kuwashika mkono wadau wa elimu kwenye wilaya hiyo.
Aidha Ndugu Kalinga amewaasa wazazi na walezi wilayani Mufindi kuhakikisha kuwa wanawapeleka wananfunzi shule, kwani elimu ni ufunguo wa maisha.
Naye Mmiliki wa kituo cha elimu na malezi kwa watoto cha Excell Bw. Isaya Juliano Kalinga, Amemshukuru mdau huyo kwani ametimiza ahadi yake kwa wakati.
Mpaka sasa Mdau Fredrick Victory Kalinga ameendelea kuwa karibu na vijana ambapo amewahi kudhamini bonanza la michezo kata ya Ihanu, Kwenye elimu ameongeza nguvu katika maendeleo ya shule ya secondary ya Lyanika sambamba na kusaidia kikundi cha kijamii cha Mkombozi kilichopo kidete Mdabulo ikiwa kwa sasa yeye ndiyo mlezi.