Tadio yawanoa wanahabari kuelekea uchaguzi mkuu
14 January 2025, 14:09
Na Juliana Mhavile
Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Wandishi wa habari wa kituo cha redio Mufindi FM 107.3, wametakiwa kuzingatia maadili yao ya kiuandishi Katika kazi yao ya kuhabarisha umma.
Hayo yamesemwa January 13, 2025 na Mhariri kutoka jukwaa la Habari mtandaoni (RADIO TADIO) Bw.Hilali Ruhundwa wakati akitoa elimu kuhusu maadili ya Waandishi wa habari katika kituo cha Mufindi FM 107.3.
Kwa upande wake Mhariri mkuuu wa kituo cha Redio Mufindi FM Bestina Nyangaro ameushukuru uongozi wa Radiotadio kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu kwa wandishi wa habari hususani kwa msimu wa uchaguzi mkuu.
Nao baadhi ya wafanyakazi katika kituo hicho wameeleza namna ambavyo elimu hiyo itawasaidia katika majukumu ya kiuandishi.
Radio Tadio ni umoja wa radio mtandao ambapo kwa Tanzania bara na Visiwani (Zanzibar) zipo radio 42 kwenye umoja wa Radio Tadio.