Wanaotegemea maji mto Ruaha wakumbukwa
16 July 2024, 21:11
MAFINGA.
Na Bestina Nyangaro
Takribani wananchi wapatao 3,200 wa kijiji cha Itimbo kata ya Rungemba halmashauri ya mji Mafinga wanatarajia kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kupata huduma ya maji ifikapo disemba mwaka huu 2024, ambapo mradi wa maji Itimbo unatarajiwa kukamilika.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi huo kwa mkandarasi, mbunge wa Mafinga mjini Cosato Chumi leo julai 16, makabidhiano ambayo yamefanyika kwenye kitongoji cha Geza Ulole, amesema kwa nafasi yake ataendelea kuisimamia serikali kutatua kero na changamoto za wananchi.
Awali akisoma taarifa ya mradi Meneja wa wakala wa maji vijijini (RUWASA) Mhandisi Happiness Mrisho, amesema mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi million 900 fedha za P for R na kutekelezwa kwa muda wa miezi 6 kwenye vitongoji 5.
Kwa upande wake mkandarasi wa mradi huo Eng. Chelesi ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chelesi General Interprisess ameahidi kutekeleza mradi kwa wakati.
Diwani wa kata ya Rungemba Samwel Mwalongo, amewaonya wanufaika wa mradi huo kutojihusisha na vitendo vya wizi na uhujumu wa miundombinu jambo linaloweza kukwamisha mradi, huku baadhi ya wananchi wakiwashkuru viongozi kwa kuwawakilisha vyema.