Mufindi FM

Mradi wa Maji wenye thamani ya Sh. Bil 48.6 Unasusua Mafinga

9 July 2024, 09:02

Naibu Waziri Wizara ya Maji Kundo Wakati alipotembelea Mradi wa Maji wa miji 28 Mafinga eneo la jeshini Changarawe yanapojengwa matenki ya Maji Mei 24 2024.Picha na Mafinga TC

Na Bestina Nyangaro

Mafinga

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano muungano wa Tanzania mh. Kassim Majaliwa amemuagiza waziri wa maji Juma Aweso, kukutana na mkandarasi wa mradi wa maji wa miji 28 Mafinga, na kusimamia mradi huo ili ukamilike haraka, ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Wziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa wakati akihutubia wananchi wa mji Mafiinga mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi huo, julai 7, 2024.

Sauti ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Awali akizungumza kwa niaba ya wananchi Mbunge wa jimbo la Mafinga, Mh. Cosato Chumi amesema mradi huo umefikia asilimia 18 hadi sasa na umekuwa ukisuasua.

Sauti ya Mbunge Cosato Chumi

Mradi huo wenye thamani ya shilling B. 48.6, unatekelezwa na mkandarasi JANDU PLUMBERS LTD chini ya uangalizi wa mkandarasi mshauri WAPCOS LTD, ulitarajiwa kukamilika mwezi julai mwaka huu na kuhudumia wakazi wa mji Mafinga.