Mufindi FM

Shilingi million 500 kuokoa wananchi Makungu kutembea km 80 kupata matibabu

9 July 2024, 08:22

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina akimkabidhi cheti Cha pongezi Diwani wa kata ya Makungu Felix Lwimbo kwa kutambua mchango wake wa kusimama maendeleo ya kata.Picha na Anthony Kuyava.

Na Bestina Nyangaro

Mufindi

Serikali imetoa Kiasi Cha shilingi million 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo Cha afya kata ya Makungu halmashauri ya wilaya ya Mufindi ili kuondoa adha kwa wananchi wapatao 17,373 kutembea umbali mrefu kupata huduma za matibabu.

soma pia Kuhusu Mufindi FM 107.3

Awali wananchi hao walilazimika kutembea umbali mrefu kupata huduma za matibabu katika hospitali ya mji Mafinga takribani kilomita 80, jambo lililohatarisha maisha yao.

Akizungumza Katika mkutano wa halmashauri kuu kata ya Makungu, Julai 5 2024 Mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina amesema hicho ndicho kilio na kiu ya wanamakungu ndiyo maana serikali imetatua changamoto hiyo.

Sauti ya Festo Mgina

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 ya Chama Cha Mapindizi ccm katani hapo, diwani wa kata ya Makungu Felix Lwimbo amesema kati ya pesa hizo wananchi wamechangia shilingi million 36 na kuongezwa kwamba Hadi sasa ujenzi umefika asilimia 86 na kitarajiwa kukamilika mwisho mwa mwezi jalai mwaka huu.

Sauti ya Felix Lwimbo

Baadhi ya wakaazi wa kata hiyo walikuwa na haya yakusema.

Sauti ya wananchi wa kata ya Makungu

Kata ya Makungu Ina jumla ya vijiji vitano ambavyo ni Mabaoni, Lugolofu, Kitasengwa, Lugema na Makungu.