Mufindi FM

Mufindi DC yapata hati safi 2022/2023

27 June 2024, 07:52

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Wakishiriki katika kikao Cha Baraza la madiwani kujadili hoja za CAG June 26 2024. Picha na Said Mlelwa.

Na Witness Alex

Mufindi

Mkuu Wa Mkoa Wa Iringa Mhe Peter Serukamba Ameipongeza Halmashauri Ya Wilaya Ya Mufindi Kwa Kupata Hati Safi Kutoka Kwa Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali (CAG) Kwa Mwaka Wa Fedha 2022/2023.

Leo Juni 26,2024 Akiwa Kwenye Mkutano Maalumu Wa Baraza La Madiwani Wa Kujadili Hoja Za Mkaguzi Mkuu Wa Serikali (CAG) Ya Mwaka 2022/2023 Katika Ukumbi Wa Halmashauri Hiyo Itulavanu Ambapo Ameongeza Kwamba Matokeo Hayo Yametokana Na Ushirikiano Mzuri Uliopo Baina Yao.

Sauti ya RC Iringa

Mhe.Serukamba Pia Ameitaka Halmashauri Hiyo Kutafuta Namna Sahihi Ya Kumaliza Miradi Yote Ambayo Haijakamilika Ili Kuwezesha Kuanzishwa Kwa Miradi Mwingine Huku Akisisitiza Ukusanywaji Zaidi Wa Mapato.

Sauti ya RC Serukamba

Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Mufindi Akizingumza Kwa Niaba Ya Uongozi Wote Amemshukuru Mkuu Wa Mkoa Huku Akiahidi Kuwa Halmashauri Imepokea Maagizo Aliyotoa Na Kuahidi Kuyatekeleza Kwa Ukamilifu.