Mufindi FM

Wawili wafariki, 16 kujeruhiwa Mafinga

16 June 2024, 11:39

Mwonekano wa gari baada ya ajali iliyokuwa wawili na kujeruhi 16, Mafinga.

Na Bestina Nyangaro

Watu wawili wamefariki Dunia na wengine 16 kujeruhiwa, wakiwemo watumishi 6 wa shirika la umeme (TANESCO) Mafinga na wakatamiti katika shamba la miti Sao Hill.

Ajali hiyo imetokea Juni 15, 2024 ikihusisha gari namba T195 EDF aina ya Mitsubishi Fuso na Mwendesha baiskel, Mganga mfawidhi hospitali ya mji Mafinga Dkt. Hamata Haule amethibitisha kupokea Miili ya watu wawili, Moja akiwa ni mtumishi wa TANESCO Evans Lusinde (37) na Mwendesha baiskel Valentino Ubeleti mkazi wa Changarawe (70), pamoja na majeruhi 16.

Dkt. Hamata amesema majeruhi wanne wamepewa rufaa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa na wengine Hali zao zinaendelea vizuri.

Meneja wa TANESCO Mafinga, Mhandisi Modest Mahururu, ameeleza kwamba watumishi wake walikuwa wakitoka katika majukumu Yao eneo la Igowole, wakiwa njiani waliombwa lifti na wakatamiti wa Sao Hill, wakiwa safarini wakapata ajali eneo la Changarawe, baada ya dereva kupoteza mwelekeo wakati akijaribu kumkwepa Mwendesha baiskel.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Alfred Mbena, amesema chanzo Cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva, na kutoa wito kwa Madereva kuzingatia Sheria za usalama barabarani.