Maafisa habari watakiwa kuandika habari za takwimu
8 October 2024, 8:07 pm
Ofsi ya takwimu hapa nchini imeandaa mafunzo ya maafisa habari na mawasilino wa mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro yanayohusu umuhimu wa kutumia takwimu sahihi katika uandaaji wa taarifa.
Na Mzidalfa Zaid
Serikali imewataka maafisa habari pamoja na waandishi wa habari kuhakikisha wanaandika habari zenye takwimu sahihi kutoka vyanzo sahihi ili kuisadia serikali kufahamu idadi ya vitu au watu.
Hayo yamesema na katibu tawala mkoa wa Manyara Mariam Muhaj ambae amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa ManyaraQqueen sendiga katika ufunguzi wa mafunzo ya maafisa habari na mawasilino wa mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro yaliyofanyika katika ukumbi wa hazina ndogo mkoani Manyara yanayohusu umuhimu wa kutumia takwimu sahihi katika uandaaji wa taarifa.
Akizungumza kwa niaba ya mtakwimu mkuu wa serikali dokta Albina Chuwa, mwakilishi kutoka ofisi ya takwimu Magreth Magana amezisistiza ofisi zinazozalisha takwimu kuzalisha takwimu kwa viwango bora ili zitumeke kama takwimu rasmi.
Kwa upande wake meneja wa tehama na uratibu wa data Mwanaidi Mawiza amesema mafunzo hayo yatakuwa endelevu nchi nzima kwa waandishi wa habari kwa kuwa wako karibu na jamii kwa kutangaza takwimu zinazotolewa na mamlaka husika.
Nao baadhi ya washiriki ambao wamepewa mafunzo hayo, wamewashukuru waandaji wa mafunzo hayo kwa kuwa yamewasaidia kufahamu namna ya kuandaa taarifa sahihi ambazo watazitoa kwa vyombo vya habari.