FM Manyara

Takukuru Manyara kudhibiti rushwa kuelekea uchaguzi

11 September 2024, 5:24 pm

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara imesema itamchukulia hatua  za kisheria mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa kipindi cha uchaguzi.

Na Mzidalfa Zaid

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara imewataka wananchi  kutojihusisha na vitendo vya rushwa kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani ili wawe na haki ya kuchagua kiongozi bora wanaemtaka.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Manyara Bahati Haule wakati akiongea na FM Manyara ambapo amesema wanataka kufanyike uchaguzi huru na kila kiongozi ashinde kwa haki na sio kushinda kwa kutoa rushwa kwa wapiga kura.

Amesema TAKUKURU mkoa wa Manyara itamchukulia hatua  za kisheria mtu yeyote atakaejihusisha na vitendo vya rushwa kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

sauti ya Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Manyara Bahati Haule

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kutoa taarifa wanapobaini uwepo wa vitendo vya rushwa, kwa kuwa taasisi hiyo inamlinda mtoa taarifa.

sauti ya Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Manyara Bahati Haule