FM Manyara

Mwenge wa uhuru wapokelewa Manyara

12 July 2024, 4:50 pm

picha ya mkuu wa mkoa Singida akikabidhi mwenge wa uhuru kwa mkuu wa mkoa wa Manyara

Vituo 2043 mkoani Manyara vinatarajiwa kutumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameendelea kutoa elimu ya uchaguzi kwa wananchi ili kuchagua viongozi bora watakao waletea maendeleo

Na Emmy Perter

Mwenge wa uhuru umepokelewa leo julay 12 wilayani  Hanang’ mkoani Manyara na mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga ukitoka mkoani Singida ambapo ukiwa mkoani hapa utazindua miradi 57 yenye  thamani ya shillingi bilioni 149.5.

Akipokea mwenge wa uhuru  katika kijiji cha gehandu wilayani Hanang’ mkoani Manyara Sendiga amesema mkoa wa Manyara umeupokea ujumbe wa mwenge wa uhuru kwa mwaka 2024 kwa kuendelea kuhamasisha wananchi kutunza mazingira na kuepuka kukata miti hovyo pamoja na kutumia nishati safi ya kupikia.

sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara

Sendiga amesema mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameendelea kutoa elimu ya uchaguzi kwa wananchi na vituo 2043 vikitarajiwa kutumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mkoa wa Manyara,

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara

AIDHA, AMEWATAKA WANANCHI  MKOANI HAPA KUJITOKEZA KWA WINGI KUULAKI MWNGE WA UHURU KATIKA MAENEO UTAKAPOKUWA UNAPITA MWENGE HUO NA KAULI MBIU YA MWENGE WA UHURU KW MWAKA HUU INASEMA TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SEREKALI ZA  MITAA KWA UJENZI WA TAIFA ENDELEVU