Sendiga amaliza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na halmashauri ya Babati Mji
11 July 2024, 5:42 pm
Mkuu wa mkoa Manyara Queen Sendiga amemuagiza mkuu wa wiliya ya Babati Lazaro Jacob Twage kwa kushirikiana na Halmashauri pamoja na serikali ya kijiji cha kiongozi kupima maeneo yote yaliyovamiwa na wananchi pamoja na kutenga ekari 375 kati ya ekari 960 zilizovamiwa na wananchi hao na kuziwekea alama pamoja na uzio ili isivamiwe tena.
Na Geogre Augustino
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amemaliza mgogoro wa wananchi wa kitongoji cha misuna na kijiji cha kiongozi kata ya maisaka Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara baada ya wananchi wa maeneo hayo kudai maeneo hayo ni yao na kuigomea serikali ya Halmashauri kuchukua maeneo hayo.
Sendiga ametatua mgogoro huo jana julay10 2024 baada ya kufika katika maeneo hayo na kuwasikiliza wananchi ambao waliandamana kudai haki yao na kumuomba mkuu wa mkoa kufika katika maeneo hayo ili kuwasikiliza ambapo amesema maeneo ambayo wananchi wanadai kuchukuliwa na Halmashauri ni ya serikali na wananchi ndio wamevamia maeneo hayo na kuanzisha makazi pamoja na shughuli za kilimo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.
Aidha Sendiga amemuagiza mkuu wa wiliya ya Babati Lazaro Jacob Twage kwa kushirikiana na Halmashauri pamoja na serikali ya kijiji cha kiongozi kupima maeneo yote yaliyovamiwa na wananchi pamoja na kutenga ekari 375 kati ya ekari 960 zilizovamiwa na wananchi hao na kuziwekea alama pamoja na uzio ili isivamiwe tena
Aidha siku chache baadhi ya kina mama wa kijiji cha kiongozi walifanya maandamano ya amani ya kutaka kuonana na mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga kutokana mgogoro wa shamba la hanadeko lililovamiwa na wananchi kwa zaidi ya miaka 20 na halmashauri ya mji wa Babati ikidaiwa kutaka kuwaondoa ili kumpatia muwekezaji eneo hilo.