Nida Manyara yatoa zaidi ya Vitambulisho laki tatu
7 March 2024, 3:56 pm
Nida mkoa wa Manyara yafanikiwa kutoa zaidi ya vitambulisho laki tatu kwa wananchi wa mkoa wa Manyara.
Na Hawa Rashid
Mamlaka ya vitambilisho vya Taifa Nida mkoa wa Manyara imeafanikiwa kutoa zaidi ya vitambulisho laki tatu kwa wananchi wa mkoa wa Manyara ambao walikuwa hawajapa tavitambulisho vyao kwa muda mrefu baada ya kufanyika kwa maboeresho na ufanisi wa utoaji wa vitambulisho.
Afisa usajili wa Nida mkoa wa Manyara Amwesiga Bandio ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na fm manyara katika kipindi cha mseto wa leo,amesema zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa mkoa wa Manyara limezinduliwa April 29 mwaka 2024,na mkuu wa mkoa wa Manyara Qeen Sendiga nakuwataka wananchi ambao waliojiandikisha Nida kufatilia vitambulisho vyao kwa watendaji wa mitaa.
Bandio amesema baada ya wiki mbili kwa ambao hawajafata vitambulisho vyao katika ofisi za watendaji wa mitaa vitarudishwa katika ofisi zao za Nida ili kuepusha vitambulisho hivyo kukaa kwa muda mrefu katika ofisi za vijiji na mitaa kwakua vitambulisho hivyo havitaweza kuisha kutokana na wengine wenye vitambulisho walishafari.
Aidha,amesema wameweka utaratibu mzuri katika ofisi za watendaji wa mitaa kwa kuweka majina ya wananchi wenye vitambulisho vyao ili kabla ya kuchukua anahakiki jina lake pamoja na kusaini ili kuchukua kitambulisho chake.