Mtoto wa miaka 7 Babati auwawa kwa kutenganishwa kichwa, kiwiliwili
20 February 2024, 7:14 pm
Na Mzidalfa Zaid
Mtoto mwenye umri wa miaka saba ambaye ni mwanafuzi wa chekechea ameuwawa kwa kuchinjwa na mtu asiyejulikana katika kijiji cha Mapea kata ya magugu wilayani babati mkoani Manyara.
Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Mapea Filmon Mbogo, amekiri kutokea kwa tukio hilo katika kijiji chake nakusema baada ya kupata taarifa hizo ameliarifu jeshi la polisi ili kupata maelekezo kuhusu mwili huo.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Mapema wamesema mtoto huyo alikuwa anasoma katika shule ya msingi Mapea, na wakati wakitoka shule walikutana na mtu wasiomfahamu ambaye aliwadanganya anakwenda kuwachumia mazambarau ambapo alimchukua mtoto huyo nakwenda kumchinja shambani kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.
Aidha, kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara George Katabazi amethibitisha kutokea kwa tukio nakusema atatolea ufafanuzi baada ya kupata taarifa kamili.