FM Manyara

Mashine 49 za mchezo wa kubahatisha zakamatwa Manyara

3 June 2024, 5:15 pm

Picha ya mashine za mchezo ya kubahatisha(Dubwi)

Kamanda  wa polisi mkoani Manyara Geogre Katabazi awataka wamiliki na wafanya biashara wa michezo ya kubatisha kuzingatia taratibu za sheria na kanuni zilizowekwa na bodi ya michezo 

Na Emmy Peter

Jeshi la polisi mkoa wa Manyara  kwa kushirikiana na maafisa kutoka bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini  wamekamata  mshine 49  maarufu kwa jina la Dubwi ambazo zilikuwa zikifanya kazi kinyume na sheria bila kuwa na leseni  na kukwepa kulipa kodi ya serikali 

Akizungumza  na wandishi  wa habari ofisini kwake kamanda  wa polisi  mkoani  mkoani Manyara George katabazi Amesema watuhumiwa watano wamekamatwa na jeshi hilo pamoja na mshine sita ambazo zilikuwa zikimilikiwa na watu wawili bila kufuata sheria za kumiliki  mshine hizo za mchezo wa kubatisha.

Sauti ya kamanda Katabazi

Aidha kamanda Katabazi amewataka wamiliki na wafanya biashara wa michezo ya kubahatisha kuzingatia taratibu za ,sheria na kanuni zilizowekwa na bodi ya michezo ikiwa ni pamoja na leseni na kuchangia pato la serikali pamoja na miongozo iliyowekwa kwa wamiliki hao.