FM Manyara

Wananchi watakiwa kutowanyanyapaa waraibu wa dawa za kulevya

22 February 2024, 6:31 pm

Viongozi wa Takukuru pamoja na DCEA wakiongea katika studio za Fm manyara

Jamii  mkoani Manyara imetakiwa kuacha tabia ya kuwanyanyapaa waraibu wa dawa za kulevya na badala yake wawaunganishe na vituo vya tiba.

Na Mzidalfa Zaida

Jamii  mkoani Manyara na Kanda ya Kaskazini kwa ujumla imetakiwa kuacha tabia ya kuwanyanyapaa waraibu wa dawa za kulevya na badala yake wawaunganishe na vituo vya tiba.

Wito huo umetolewa leo na  afisa ustawi jamii kutoka mamlaka ya dawa za kulevya kanda ya kaskazini Sara Ndaba, wakati akiongea na Fm manyara, amesema kuna baadhi ya waraibu wa dawa za kulevya ambao wanatengwa na jamii kutokana na namna wanavyoathirika.

sauti ya afisa ustawi wa jamii dcea

Aidha, afisa elimu jamii dcea kanda ya kaskazini Shabani Miraji, amesema dawa za kulevya zinaweza kuleta madhara makubwa ikiwemo kutenda matendo yasiyokubalika katika jamii.

Shabani miraji afisa elimu jamii DCEA kanda ya kaskazini madhara ya dawa za kulevya

Kwa upande wake afisa takukuru mkoa wa Manyara Rchard Samila, ameelezea namna Takukuru inavyoshirikiana namamlaka ya dawa za kulevya kupambana na vitendo vya rushwa na dawa za kulevya.

Richard Samila afisa TAKUKURU