Matokeo ya Sensa yasaidia kukuza uchumi
1 May 2024, 10:25 am
Viongozi wa serikali, watendaji, makundi maalum na viongozi wa kimila na siasa mkoa wa Manyara watakiwa kuyatumia matokeo ya sensa ya watu na makazi katika fursa mbali mbali za kiuchumi na biashara
Na George Augustino
Kamisaa wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 anna makinda amesema matokeo ya sensa yana umuhimu mkubwa kwa wananchi kujua fursa mbalimbali za kiuchumi na biashara nakuisaidia serikali kutambua maeneo yenye uhitaji wa huduma mbalimbali za kijamii kama elimu,afya na maji.
Makinda ameyasema hayo leo katika mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi kwa viongozi wa serikali, watendaji, makundi maalum na viongozi wa kimila na siasa mkoa wa Manyara iliyofanyika katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi Ccm mjini Babati mkoani hapa .
kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro twange ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga ameishukuru ofisi ya Taifa ya Takwimu Nbs kwa kukubali ombi la kufanya mafunzo ya matumizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 mkoani hapa
Naye mratibu wa sensa ya watu na makazi kitaifa Seif Kuchengo amesema sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 imelata sifa kwa Taifa na kurekodi idadi yote ya wanainchi ikiwemo jamii ya wafugaji, tofauti na nchi nyingine ambazo haziwajumuishi wafugaji katika sensa ya watu na makazi.
Aidha,mratibu wa mafunzo hayo ambaye ni mbunge wa viti maalumu mkoa wa Manyara Rejina Ndege amewataka wajumbe walioshiriki mafunzo hayo ya matumizi ya sensa kuyatumia vizuri na kutoa elimu kwa watu wengine.