Rc Sendiga asema ulinzi na usalama umeimarishwa katika sikukuu za mwisho wa mwaka
24 December 2024, 5:43 pm
Picha ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga
Sendiga awataka wazazi na walezi kuwa na uangalizi wa karibu na watoto wao na kuacha kuwapeleka katika maeneo yasiyo rasmi zikiwemo kumbi za starehe katika msimu wa sikuku nakusema mkoa wa Manyara bado upo katika wimbi kubwa la ukatili wa kijinsi.
Na Emmy Peter
Katika kuelekea sikukuu za Chrismas na mwaka mpya mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema ulinzi na usalama umeimarishwa ambapo amewahimiza wananchi kusherekea kwa amani utulivu katika sikuku hizo za mwisho wa mwaka .
Sendiga amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amesema mkoa wa Manyara bado upo katika wimbi kubwa la ukatili wa kijinsia ambapo amewataka wazazi na walezi kuwa na uangalizi wa karibu na watoto wao na kuacha kuwapeleka katika maeneo yasiyo rasmi zikiwemo kumbi za starehe katika msimu wa sikuku.
Aidha,Sendiga amesema katika msimuu huu wa likizo mzazi anawajibu wa kumwagalia mtoto wake hasa watoto wa shule za bweni na kufahamu tabia ya mtoto kabla ya likizo kuisha kwani itasaidia kuondokana na tabia ambayo anajifunza kutoka kwa wenzake.