FM Manyara

Sendiga katika foleni kujiandikisha daftari la mkazi.

11 October 2024, 6:34 pm

Picha ya Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga akijiandikisha katika daftari la mkazi katika mtaa wake wa Mrara.

Zoezi la kujiandikisha katika daftari la mkazi katika mtaa wa mrara kata ya Babati wilayani Babati mkoani Manyara limeanza rasmi leo  ambapo wananchi  wametakiwa kujitokeza katika zoezi hilo ili watimize haki yao ya kikatiba ya  kuchagua viongozi wao wa  mtaa wanaowahitaji kuwaongoza

Na George Augustino.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka wananchi wote wa mkoa wa manyara kujitokeza kwa kujiandikisha katika daftari la mkazi ambalo limeanza leo octoba 11, 2024 hadi octoba 20 mwaka huu kwaajili ya kuchagua viongozi wa serikali za vijiji na mitaa uchaguzi utakaofanyika novemba 27, mwaka huu.

Sendiga ametoa wito huo leo aliposhiriki zoezi la kujiandikisha katika daftari la mkazi katika mtaa wa mrara kata ya Babati wilayani Babati mkoani hapa ambapo amewataka wananchi wengine kujitokeza katika zoezi hilo ili watimize haki yao ya kikatiba ya  kuchagua viongozi wao wa  mtaa wanaowahitaji kuwaongoza.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa manyara

kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa mrara Godfrey Bayo amesema wameendelea kuwasisitiza wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari hilo la mkazi kwa kupiga debe na kupita nyumba kwa nyumba kuwakumbusha wananchi wote wenye sifa za kijiandikisha kushiriki zoezi hilo ambalo nila mda mfupi.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa mrara