Sakata la Gekul lapigwa kalenda
22 March 2024, 4:27 pm
Mbunge wa Babati mjini Pauline Gekul kusomewa hukumu ya rufaa ya jinai April 5, 2024
Na mwandishi wetu
Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Manyara imepanga Aprili 15,2024 kusoma hukumu ya rufaa ya jinai iliyokatwa na Hashim Ally dhidi ya Mbunge wa Babati mjini Pauline Gekul, baada ya majibu ya rufaa hiyo kutopewa wito wa kuitwa Mahakamani.
Rufaa hiyo namba 577/2024 imesikilizwa na jaji Devotha Kamuzora, baada ya Ally kupinga uamuzi uliofanywa na Mahakama ya wilaya ya Babati Desemba 27,2023 ya kuiondoa kesi ya jinai baada ya Mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo ambayo Ally alidai kushambuliwa mwili nakufanyiwa ukatili na Mbunge huyo.
kabla ya kusikilizwa rufaa hiyo, Mahakama hiyo ilisikiliza pingamizi za awali zilizowasilishwa na upande wa mjibu maombi, kisha kusikiliza hoja sita zilizowasilishwa na upande wa mleta rufaa.
Gekul ambaye alikuwa Naibu waziri wa katiba na sheria kabla ya kutenguliwa wadhifa huo Novemba 25,2023, alidaiwa kumshambulia na kumdhuru Hashim Ally Novemba 11,2023 kinyume cha kifungu cha 41 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 ya 2022.