Radio Fadhila

Miradi iliyoahidiwa kwenye ilani yatekelezwa

9 October 2024, 10:44 PM

pichani ni Mwenyekiti CCM Wilaya ya Masasi

Na Lilian Martin.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Masasi Bi.Mariam Kasembe amewahakikishia Wananchi wa Masasi kuwa miradi mingi ambayo ilihaidiwa kwenye ilani ya utekelezaji wa CCM kwamba miradi hiyo imeenda vizuri na kwamba wao viongozi ambao wanasimamia wanakiri kuona kazi kubwa imefanyika.

Bi.Kasembe ametoa kauli hiyo katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika jengo la Zahanati Maparawe iliyopo Katika kata ya mchauru Halmashauri ya Wilaya Masasi Oct 9,2024.