Radio Fadhila

Shule maalum Lukuledi watembelewa na Upendo charity

2 October 2024, 10:46 AM

Bi Christine simmo akiwa na wanafunzi shule ya watoto wenye mahitaji maalumu Lukuledi

Na. Lilian Martin

shirika lisilo la kiserikali Upendo charity limetembelea shule ya watoto wenye mahitaji maalum Lukuledi kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya watoto wenye ulemavu waliopelekwa na shirika hilo lakini pia walipata nafasi ya kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia.

hata hiyo Bi simmo aliwataka wanafunzi hao wajue nini kusudi la wao kuwa hapo wajue umuhimu wa Elimu na kutambua faida zake

Sambamba na hayo Bi. Simmo aliwataka waalimu kuwa msaada wa karibu kwa watoto kama walinzi na kuwaonyesha upendo zaidi ili wajisikie wapo sawa kama watoto wengine

wakishiriki chakula cha mchana pamoja

licha ya kutoa elimu hiyo pia alishiriki chakula cha pamoja na wanafunzi katika shule hiyo maalumu na kufurahi nao pamoja.