Radio Fadhila

Kilimo cha Mavundu chatoa tumaini kwa wakulima Nachingwea

27/03/2026, 14:11

Akizungumza

Kilimo ni uti wa mgongi huu ni msemo uliotumiwa tangu enzi za kale na hadi leo msemo huu unaishi ndani ya jamii zetu na kutambua umuhimu wa kilimo katika maisha

Na. Faraja Membe

Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG), kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Leeds cha Uingereza na wadau wa kilimo wilayani Nachingwea, tarehe 24–25 Machi 2026 wameendesha warsha ya siku mbili kuwasilisha matokeo ya utafiti wa kilimo cha mavundu, mfumo unaolenga kuongeza tija ya uzalishaji na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mradi huo ulioanza mwaka 2024 unatekelezwa katika vijiji vya Kilimarondo, Namatunu na Kiegei B, ukihamasisha matumizi ya mbinu endelevu ya kuacha ardhi ipumzike ili kurejesha rutuba na kudhibiti magugu.

Akizungumza

Wataalamu wanasema kilimo hicho kina mchango mkubwa katika kuhifadhi mazingira kwa kufyonza hewa ukaa na kupunguza utegemezi wa mbolea za viwandani, huku wakulima wakionesha matumaini makubwa ya kuboresha uzalishaji na kupunguza migogoro ya matumizi ya ardhi.