Radio Fadhila
Radio Fadhila
20/03/2026, 13:32

Kata mti panda mti ni neno tunalolisikia mara nyingi ikihimiza umuhimu wa miti katika maeneo yetu kwa lengo la kutunza uoto wa asili je wewe ni miongoni wa wanao panda au wanaokata?
Na Lilian Martin
Kufuatia Siku ya Misitu Duniani yaliyofanyika mkoani Lindi na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Emmanuel Nchimbi ambapo amesema zoezi la upandaji miti liwe endelevu katika mikoa yote nchini.

Karibu tusikilize kipindi cha fadhila mseto ambapo leo March 19 tumeweza kuzungumzia habari hiyo kuhusu misitu na kuzungumza na Timotheo Abeli ambaye ni Mhifadhi Misitu mkuu wilayani Masasi
Wakati mazungumzo hayo yaliendelea katika studio za Radio fadhila tumewagusa wauza mkaa ambao wao ni moja ya watu wambao hafanya shughuli zao katika misitu
Lakini kuna msikilizaji wa Radio alizungumza nasi kwa njia ya simu kuhusu kutoa elimu kwa wauza mkaa
Mhifadhi misitu Bwn Timotheo Abeli ameongeza kwa kusema tuhamasike kutunza Misitu