Radio Fadhila

Kikosi cha Ulinzi na usalama wanawake Masasi cha mgusa Mgane

11/03/2026, 13:24

Kikosi cha ulinzi na usalama wanawake

Matendo ya huruma ni vitu vinavyo leta faraja katika jamii kwa kusaidia mtu mwenye uhitaji hali hii huongeza tabasamu kwa aliyefikiwa na matendo hayo

Na Lilian Martin.

Kikosa cha ulinzi na usalama Wilayani Masasi kimemtembelea mwanaume anaye fahamika kwa jina la Raphael john anayeishi kijiji cha mbonde Wilayani Masasi ambaye amefiwa na mkewake na kumuacha na mtoto mdogo

Mwanaume huyo alizungumza na kueleza kwamba mke wake alifariki kwa tatizo la uzazi wakati wa kujifungua ndio maana amebaki akimlea mtoto huyo akisaidiwa na dada yake

Kikosi cha ulinzi wakiwa na baba na mtoto kendrick
Mgane na dadayake wakizungumza

Kikosi hicho kilitoa msaada vitu kwa Bwana Raphael john kama unga,makopo ya maziwa sabuni na vitu vingine pamoja na Fedha,

Baadhi ya vitu walivyo vitoa

kwa upande wake kiongozi wa msafara huo alizungumza machache wakati akikabidhi kiasi cha fedha kwa baba wa mtoto kendrick

Akizungumza wakati wa kukabidhi